Mshambuliaji wa klabu ya PSG Neymar ameitaka klabu yake mpya kumuuza mshambuliaji mwenza Edinson Cavani baada ya wawili hao kuzozana kuhusu kupiga mkwaju wa penalti.
Raia huyo wa Brazil pamoja na mwenzake wa Uruguay walilazimika kutawanywa katika chumba cha maandalizi kufuatia majibizano makali ya mechi ya siku ya Jumapili ambapo klabu hiyo iliibuka mshindi dhidi ya Lyon.
Na sasa kulingana na gazeti la Spanish Outlet Sport, mchezaji ghali zaidi duniani amemtaka mwenyekiti wa klabu hiyo Nasser Al-Khalifi kumuuzilia mbali mwenzaki akisema kuwa uhusiano wake na Cavani umeharibika na hivyobasi hawawezi kucheza pamoja.
Inaaminika kwamba Neymar anataka mshambuliaji huyo kuuzwa wakati wa kufunguliwa kwa dirisha la uhamisho mwezi Januari.
Tatizo lilitokea kunako dakika ya 79 wakati ambapo Kylian Mbappe alikuwa amejishindia penalti baada ya kufanyiwa madhambi ndani ya eneo hatari.
Neymar alitaka kuipiga penalti hiyo badala ya mpiga penalti wa kila mara Edison Cavani.
Raia huyo wa Uruguay ambaye hapo awali alikuwa amehusika katika mgogoro na mchezaji mwengine wa Brazil Dani Alvez kuhusu kupiga mkwaju wa adhabu kabla ya raia huyo wa Brazil kumpatia mpira huo Neymar, alikataa katakata kabla ya kupiga penalti hiyo ambayo iliokolewa.
Cavani baadaye alimuandama Neymar baada ya mechi kabla ya wachezaji wenza Thiago Motta na Marquinhos kuingilia kati na kuwatawanya.
No comments: