NEY WA MITEGO AMTOREA POVU ALIKIBA.AKIRUDI TENA TUTAMSAHAU...

Image result for ney wa mitego
Msanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego amefunguka mambo kadhaa kuhusu mtindo wa baadhi ya wasanii kukaa muda mrefu bila kutoa ngoma.
Rapper huyo ambaye ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Makuzi’, katika mahojiano na Papaso ya TBC Fm amesema muziki wa sasa umebadilika na msanii atakayejaribu kufanya hivyo tena atapotea kabisa.
Image result for alikibaHuo muda umeisha this time mtu akirudia hivyo tena!!, yaani tutamsahau kabisa, game hilo haina tena,” amesema Nay.
Hata hivyo hajaeleweka kama jibu hilo lilimlenga msanii Alikiba ambaye alikaa kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kutoka wimbo kwani swali lilihoji; Unazungumziaje tabia ya wasanii kukaa zaidi ya mwaka bila kutoa nyimbo?.

No comments: