Mh. Temba adai Yamoto Band ilisambaratishwa na wenye fedha

Image result for yamoto band pictures
Temba ambaye alikuwa msamamizi na mmoja ya waanzilishi wa kundi hilo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa imekuwa kawaida watu kuona vipaji viking’aa ndipo wanajitokeza kwa mgongo wa kusaidia lakini hawataki kuibua vyao na ndicho kilitokea kwa Yamoto Band.
“Mimi nakupa mfano hawa Yamoto, utaona labda kuna mtu anasimamia msanii fulani, mbona hakumchukua mwanzo wakati hajulikani kabla hatujamkuza na kuwa superstar,” amesema Temba.
“Huyo mtu kama ana uwezo kwanini asingekuwa na vipaji vyake, wewe unaona tayari nuru inang’aa unaenda kuchomoa pale,” ameongeza.
Kundi la Yamoto Band ambalo liliundwa na Aslay, Beka Flavour, Marombosso na Enock Bella kwa sasa kila mmoja anafanya kazi na menejiment yake

No comments: