Mad Ice amchana Harmorapa

Image result for hamorapa picha
Msanii Mad Ice ambaye kwa muda mrefu alikuwa kimya kwenye game ya bongo fleva, ameibuka na issue ya kumpondea Harmorapa, akisema msanii huyo hafai kuwa msanii.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mad Ice amesema kwa upande wake anamuona Harmorapa kama msanii wa vichekesho, hivyo mtu akisema anafanya muziki anamuona ana matatizo ya akili.

"Nimesikia hilo jina Harmorapa nikasikitika sana, kwa sababu kuna vitu tunaharibu sanaa yetu wenyewe, kuna wasanii wanahitaji kupewa fursa,  mimi nimemuona kama mchekeshaji, ukiniambia ni comedian nitaheshimu lakini unaponiambia unamlinganisha na mimi nitakuona una kitu kinakusumbua kichwani”.

Kauli hiyo ya Mad Ice sio mara ya kwanza kusikika kwani hata producer mkongwe bongo Master Jay, aliwahi kuzungumza kuwa Harmorapa hastahili kuitwa msanii wa muziki kwani hajakidhi sifa, isipokuwa ni sawa na mchekeshaji.

No comments: