Kipande cha ndege ya KLM chaanguka na kuharibu gari vibaya Japan


Kipande cha ndege ya KLM chaanguka na kuharibu gari vibaya Japan 
Gari moja kwenye mji wa Osaka nchini Japan limeharibiwa vibaya wakati kipande cha bawa la ndege kiliiangukia kutoka umbali wa zaidi ya mita 2000 angani.
Kipande hicho kilichokuwa na uzito uliozidi kilo 4, kilianguka kutoka ndege ya shirika la KLM Royal Dutch, wakati ndege hiyo ilikuwa ikipaa, na kuharibu vibaya upande wa nyuma wa kioo cha gari na pia paa lake.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Ndege hiyo ya Boeng 777 iliyokuwa imebeba zaidi ya abiria 300 ilitua salama katika uwanja Schiphol mjini Amsterdam Jumamosi jioni.
KLM inasema kuwua inajutia kisa hicho na imeanzisha uchunguzi.

No comments: