mitandao ya wahalifu wanaosafirisha pembe za faru kutoka barani Afrika, wanabadilisha penbe hizo kuwa vito ili kukwepa kutambuliwa katika viwanja vya ndege.
Shirika la kufuatilia biashara inayohusu wamyamapori imefuchua kuwa pembe hizo hutengenezwa kuwa bangili, mikufu na hata kusawa na kuwa unga.
Mchunguzi mkuu aliiambia BBC kuwa sasa bishara ya pemba za faru imegeuzwa na kuwa biashara ya vitu vya stahere.
Takriban faru 7,100 wanakadiriwa kuuliwa barani Afrika tangu mwaka 2007.
Laeo hii karibu faru 25,000 ndio walisalia.
"Ni jambo la kusikitishaa, kwa sabua ikiwa mtu atatembea akipitia uwanja wa ndege akiwa amevaa mkufu ulitengenezwa kutoka kwa pembe ya faru, ni nani atamzuia? alisemaa Julian Ridemeyer.
Masoko ya pembe za faru yanabaki kuwa yale yale, soko kubwa zaidu likiwa ni China na Vietnam.
Kumiliki pembe ya faru hasa kwa watu matajiri nchini Vietman ni kitu cha heshima kubwa
No comments: