Hii Hapa Taarifa Mpya kutoka Kwenye Kambi Ya simba sc Asubuhi Hii

Simba-SC-Logo
Kwa muujibu wa taarifa kutoka katika kambi ya Simba sc zinaeleza kua. Afisa Habari wa klabu ya Simba Sc ameendelea kutilia mkazo kuhusu taarifa za kuondoka kwa kocha wake mkuu, Joseph Marius Omog.

 Manara amefunguka na kusema kua klabu hiyo haina mpango wa kuachana na kocha huyo wala benchi la ufundi la klabu hiyo kwa sasa.“Nimekwishaeleza tangu awali kwamba, hakuna mechi tano wala huo mpango wa kumuondoa kocha Omog au benchi zima la ufundi, klabu ya Simba haina mpango huo".


Hata hivyo amewataka, wapenzi na Wanachama wa klabu hiyo  kua na imani na uongozi na benchi zima la ufundi la klabu hiyo.


Huyu hapa tena :- “Tunawaomba mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba kuweka imani yao kwa uongozi, kikosi cha Simba na benchi la ufundi tunajua nini mashabiki wetu wanachotaka na ndicho tunachopambana kuhakikisha tunafikia malengo,” alisema Manara.

No comments: