Msanii wa Tanzania Diamond Platnumz ameomba radhi baada ya kupata mtoto nje ya ndoa na mwana mitindo wa taifa hilo Hamisa Mobetto ambaye alishiriki katika kanda yake ya muziki.
Katika mahojiano na idhaa moja nchini humo nyota huyo alifumbua fumbo la muda mrefu lililokuwa likiwakera mashabiki wake wengi kuhusu uvumi uliokuwa ukisambaa kuhusu uhusiano wake na Hamisa.
Diamond ameomba radhi kwa mkewe mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan na familia yake.
''Ningependa kuomba radhi kwa mke wangu na watoto kwa makosa hayo'', alisema katika mahojiano.
Bi Mobetto alishiriki katika video ya wimbo wa Diamond Salome ambao umegonga vichwa vya habari na kupendwa na mashabiki wengi wa muziki katika eneo la Afrika mashariki.
- Diamond auza njugu karanga
- Diamond ampeleka mkewe Mombasa kumliwaza
- Diamond na Harmonize washinda tuzo Marekani
Katika mahojiano hayo Diamond alisema kuwa alimjua kipusa huyo kwa miaka saba na kwamba walikuwa na uhusiano ambao haukuendelea kati ya mwaka 2009-10 kabla ya kukutana na Wema Sepetu na mkewe Zari Hassan.
Anasema baadaye walikutana tena na kuanza uhusiano wakati ambapo Diamond tayari alikuwa amefunga ndoa na mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan.
''Tuliendelea na uhusiano wetu na ndiposa akawa mjamzito, lakini nilimwambia kwamba niko tayari kumuangalia mtoto lakini ajue kwamba mimi tayari nina familia kwa hivyo iwe siri yetu mimi na yeye, alisema Diamond.
Diamond anasema kwamba kulianza kuzuka uvumi katika mitandao ya kijamii kuhusu ujauzito aliokua nao na alipoulizwa iwapo alikuwa akitoa siri hiyo alikataa katakata.
Msanii huyo anasema kuwa amekuwa akimpatia bi Hamisa shilingi 70,000 za Kitanzania kilia siku mbali na kumnunulia gari jipya aina ya RAV 4 ili kumuangalia mtoto.
No comments: