Wema Sepetu na Idris.
Akizungumza na Risasi Jumamosi Wema, alisema kuwa pamoja ya kuwa alimuomba msamaha Idriss kwa kutokwenda kwenye shughuli yake ya uzinduzi wa viatu lakini hakuwahi kumpelekea ua kama walivyomsingizia na ni maneno yaliyomkera kwani yamemsababishia kugombana na mpenzi wake ambaye alihisi ni ukweli na sakata hilo lilimliza sana.
“Jamani niliumia sana kuona vile kitu ambacho sijafanya mimi kabisa na sijaelewa kwa nini walinifanyia hivyo, nilikuwa kwenye wakati mgumu sana na mpenzi wangu ambaye nilikuwa naye maana hakuweza kunielewa kabisa.
“Vitu vingine vinauma jamani nilijisikia vibaya sana ilibidi nijifungie na kulia kwa uchungu mno kwa sababu nilijua wazi mtu wangu asingependa hata kidogo na hata jamii yangu maana ningeonekana ni mtu nisiyekuwa na msimamo hata kidogo” alisema Wema.
No comments: