Amber Lulu achomoa beef na Gigy Money, aanika ukweli ‘unajua watoto wa kike tuna mambo mengi’
Labels:
Udaku
Msanii wa muziki na video vixen Bongo, Amber Lulu amedai kuwa hana beef na Gigy Money kama ambaavyo imekuwa ikiripotiwa mtandaoni
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Only You’ amesema ni kweli wamewahi kungombana na ni kitu cha kawaida kutokea ila kwa sasa ni marafiki na wanashirikiana katika kazi.
“Hapana hatuna upinzani, ni mshikaji, sisi ni marafiki wa siku nyingi ambapo kugombana ni vitu vya kawaida hata glass huwa zinagongana, halafu unajua watoto wa kike tuna mambo mengi,” Amber Lulu ameiambia Bongo5.
“LakinI sasa hivi Gigy ni mtu ambaye ni rafiki yangu, tunashirikiana katika kazi, tunashauriana, nadhani hata muziki umetufanya tuwe serious zaidi, kwa hiyo urafiki wetu mara nyingi ni kufanya kazi si kama ilivyokuwa before,” ameongeza.
Amber Lulu na Gigy Money walikuwa video vixen ila kwa sasa wote wameamua kuingaia katika muziki wa Bongo Flava
No comments: