Ivana Trump (kulia) alisema kwamba yeye ndiye Mama wa Taifa
Msemaji wa Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump ameeleza tamko la mke wa zamani wa Donald Trump Ivana kuwa "ya kujitafutia makuu na kelele za kutaka kujifurahisha".
Ivana Trump alikuwa amesema kwenye kipindi cha Good Morning America cha runinga ya ABC kwamba yeye ni "kimsingi mke wa kwanza wa Trump, mimi ni mama wa taifa".
Alisema huwa ana namba ya simu ya moja kwa moja White House lakini kwamba huwa hataki kupiga simu mara kwa mara huko kwa sababu hangependa kusababisha "wivu wa aina yoyote".
Mke huyo wa kwanza wa Trump anavumisha kitabu chake kwa jina Raising Trump (Kumlea/Kumuinua Trump), ambacho kitaanza kuuzwa Jumanne.
Aliolewa na Donald Trump mwaka 1977 lakini walitalakiana miaka ya 1990 baada ya Trump kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye angekuwa mke wake wa pili, Marla Maples.
Ivana na Donald walijaliwa watoto watatu - Donald Jr, Ivanka na Eric Trump.
Ivana Trump aliambia GMA kwamba huwa anawasiliana na mume wake wa zamani angalau mara moja kila wiki mbili.
"Nina namba ya simu ya moja kwa moja White House, lakini huwa sitaki kumpigia (Trump) akiwa huko kwa sababu Melania yuko huko,2 amesema.
"Sitaku kusababisha aina yoyote ya wivu au jambo kama hilo kwa sababu kimsingi mimi ni mke wa kwanza wa Trump. Mimi ni mama wa taifa, Sawa?"
Melania Trump alijibu kwa ukali kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Stephanie Grisham.
"Bi Trumpameifanya ikulu ya White House kuwa nyumbani kwa [mwanawe wa kiume] Barron na Rais," taarifa hilo imesema.
"Hupenda sana kuishi Washington, DC na anachukulia kuwa heshima kubwa kwake kuwa Mama wa Taifa wa Marekani. Anapanga kutumia cheo na majukumu yake kuwasaidia watoto, na si kuuza vitabu.
"Ni wazi kwamba hakuna chochote cha maana kutoka kwa mke wake huyo wa zamani. Inasikitisha kwamba anajitafutia tu makuu na kutaka kelele za kutaka kujifurahisha kwa kelele zake mwenyewe."
Majibizano hayo ni ya kwanza kutokea hadharani kati ya mke wa zamani wa rais na Mke wa Rais.
Kabla ya Trump, Ronald Reagan alikuwa rais pekee ambaye aliwahi kumpa talaka mke wake.
No comments: