Ujeruman yasherekea ndoa ya jinsia moja


Baada ya kupingwa kwa muda mrefu sheria ya ndoa ya wapenzi wa jinsia moja hatimae Ujerumani imeshuhudia tukio la kihistoria nchini humo kwa mashoga wawili waliodumu kwenye mahusiano yao kwa miaka 36 kwa kufunga ndoa leo mjini Berlin.
Bodo Mende na Karl Kreile wakila kiapo kanisani.

Tukio hilo la kufunga ndoa kwa mashoga hao wawili waliotambulika kwa majina ya Bodo Mende (60) na Karl Kreile (59), limekuja miezi michache baada ya bunge nchini humo kupiga kura ya kuruhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Awali wapenzi wa jinsia moja nchini Ujerumani walikuwa wakisajili uhusiano wao tangu mwaka 2001, hadi mwezi Juni mwaka huu wakati bunge lilipopiga kura ya kuwepo usawa wa ndoa jinsia moja.
Hata hivyo hatua hiyo ya Bunge kuruhusu ndoa ya jinsia moja haukuungwa mkono na Kansela wa Ujerumani, Bi Angela Merkel pamoja na baadhi ya wabunge wa chama chake cha CDU huku vyamala pinzani vikipiga kura kwa wingi kuruhusu ndoa ya jinsia moja.
Sherehe hizo za ndoa ya jinsia moja hazikuishia kwa wananchi tu kwani hata Msemaji na Mwenyekiti wa Chama cha haki za wanawake nchini humo Bi. Anja Kofbinger amepongeza wanandoa wengine wa kwanza wanawake (Wasagaji) huku akisema kuwa safari iliyokuwa ikisubiriwa tayari imeanza.
Daniela & Gerlinde sind das erste Berliner Frauenpaar. Hurra & herzlichen Glückwunsch
#Ehefueralle
12:26 PM - Oct 1, 2017
5 26 93 Anja Kofbinger
@AnjaKofbinger
Kwa mujibu wa takimu zilizotolewa na Yahoo mpaka sasa hivi nchini Ujerumani kuna watu 94,000 ambao wamejisajili kuwa wanahusika na mapenzi ya jinsia moja na wote wanatarajiwa kufunga ndoa,
Ndoa za jinsia moja zitawaruhusu wapenzi hao kupata haki sawa ikiwemo ya kuasili watoto kama ndoa za kawaida zinavyofanya.

No comments: