KIUNGO mkabaji wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi raia wa DR Congo, jana Alhamisi alikuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii baada ya kuzagaa kwa video yake fupi aliyojirekodi akiwa chumbani huku akiimba pamoja na kucheza.
Tshishimbi aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na umahiri wake wa kukaba, alikuwa gumzo kutokana na mazingira ya video hiyo ambayo inamuonyesha aking’ata midomo pamoja na kukata viuno kitendo ambacho kilipokelewa vibaya na baadhi ya mashabiki.
Mashabiki hao walimshambulia kiungo huyo kutokana na kitendo hicho kwa kusema kuwa hakistahili kufanywa na mtu kama yeye ambaye ni miongoni mwa wachezaji wenye majina makubwa kwa sasa hapa nchini.
Nyota huyo aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea Mbabane Swallows ya Botswana, wikiendi iliyopita hakuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichocheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ulimalizika kwa suluhu. Mechi hiyo ilipigwa Uwanja wa Uhuru, Dar.
Championi Ijumaa, lilifanya jitihada za kumtafuta kiungo huyo ili aiongelee video hiyo, lakini juhudi zake ziligonga mwamba.
No comments: