Kiungo wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya FC Barcelona, Andres Iniesta Lujan ameingia mkataba wa kudumu kuendelea kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake jimbo la Catalonia.
Iniesta amesaini mkataba wa kudumu ndani ya kikosi hicho leo siku ya Ijumaa Camp Nou.
Kiungo huyo wa Hispania amecheza jumla ya michezo 639 katika kikosi cha Barca na kushika nafasi ya pili kwa wachezaji wa timu hiyo waliyocheza maranyingi zaidi.
Andres Iniesta amefunga jumla ya mabao 55 tangu alipojiunga na kikosi cha wakubwa cha Barcelona October 29 mwaka 2002.
Tangu mwaka 2015, Iniesta amekuwa nahodha namba moja wa timu hiyo na kuwa mmoja wa alama ya klabu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, alijiunga na Klabu Barcelona mnamo Septemba mwaka 1996, akiwa na umri wa miaka 12.
Iniesta na Leo Messi ni wachezaji pekee ambao historia zao zilingana ndani ya Barca.

No comments: