Hii ndo Ahadi ya Simba kwa mashabiki zake...


KIKOSI cha Simba kinatarajia kuanza mazoezi leo kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, unaotarajiwa kupigwa Jumapili Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, huku Wekundu wa Msimbazi hao wakiwapa ahadi nono mashabiki wao.

Ahadi hiyo si nyingine, bali ni ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar mwishoni mwa wiki hii, lakini pia timu hiyo kuendelea kutoa vipigo katika mechi zao zote zijazo na hatimaye kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

Akizungumza nasi jana, Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, alisema anaifahamu vilivyo Mtibwa ikiwa ni timu nzuri, hivyo lazima wajihami ili wasije kufanya makosa na kujikuta wakishindwa kuzoa pointi zote tatu.

“Baada ya kurejea Dar es Salaam na kuwapa wachezaji mapumziko ya siku tatu, kesho (leo) asubuhi tunatarajia kuanza mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi (uliopo Kurasini, Dar es Salaam), yakiwa ni maandalizi ya kukutana na Mtibwa Sugar,” alisema.

Alisema anafahamu mchezo huo utakuwa mgumu, hivyo watapambana kuhakikisha wanaendelea kuongoza ligi na kutowapa nafasi wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa.
Kocha huyo raia wa Cameroon, alisema anatarajia kutumia mazoezi hayo kuwajenga wachezaji wake, huku akifanyia marekebisho baadhi ya kasoro zilizojitokeza katika mechi zilizopita.

Alisema malengo yao makubwa ni kutwaa ubingwa, hivyo ili wafanikishe hilo ni lazima washinde mechi dhidi ya timu kama Mtibwa ambayo ni moja ya timu ngumu.

Simba inaongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa imejikusanyia pointi kumi na moja, sawa na Mtibwa Sugar pamoja na Azam, timu hizo zikitofautiana kwa idadi ya mabao kufunga 

No comments: