MSHAMBULIAJI Mbrazil, Neymar ameitaka UEFA kuifungia Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kugoma kumlipa posho yake Pauni Milioni 23 kwa mujibu wa taarifa nchini Hispania.
Mbrazil huyo ameshauriwa na Wanasheria wake kuchukua hatua kali dhidi ya klabu yake hiyo ya zamani kwa kugoma kumlipa Pauni Milioni 23 kufuatia kuhamia Paris Saint-Germain msimu huu.
Na gazeti la AS la Hispania limeripoti kwamba UEFA iliyakataa maombi hayo ya Neymar haraka sana kutaka Barcelona iondolewe kwenye michauno hiyo ya Ulaya.
Uhamisho wa Neymar wa Pauni Milioni 198 kwenda PSG ulizuiwa hadi Agosti, hivyo baba yake Mbrazil huyo alijua atapata malipo Lakini Barcelona imegoma kufanya malipo hayo ya posho za Neymar ambayo yamo katika mkataba na Msemaji wa klabu amesema kwamba alipoteza haki za kulipwa baada ya kusajiliwa na klabu nyingine.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Barcelona, Raul Sanllehi, aliyechangia kwa kiasi kikubwa Neymar kutua katika kalbu hiyo, ameondoka Nou Camp.
Marca limeripoti kwamba Sanllehi alijitolea mno kwa maslahi ya Barcelona, lakini akaondoka amekasirishwa baada ya Neymar kuhamia PSG.
Neymar amekuwa na mwanzo mzuri katika maisha yake ya Paris tangu ajiunge na klabu hiyo kwa dau la rekodi ya dunia, akifunga mabao nane katika mechi nane za mwanzo kwenye mashindano yote.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa sasa yupo Brazil kwa majukumu ya kimataifa na amelalamikia hali hiyo baada ya sare ya 0-0 na Bolivia, iliyochezwa kiasi cha futi 12,000 juu ya kiwango cha bahari.
Baada ya mechi hiyo Uwanja wa Hernando Siles mjini La Paz, Neymar alisema ilikuwa 'ovyo kucheza kwenye hali ile, Uwanja, urefu, mpira...kila kitu kibaya,"'. hayo baada ya Julai 31.
No comments: