Kocha alimwa kadi nyekundu kwa kuzurula ovyo uwanjani
Kilimanjaro. Mchezo wa SDL kati ya AFC Arusha na Pepsi zote za Arusha uliochezwa Jumatatu katika Uwanja wa Ushirika na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, umeibua malalamiko baada ya mwamuzi wa kati kudaiwa kuharibu mchezo huo, huku kocha wa AFC akilimwa kadi nyekundu.
Mwamuzi Goodluck Simba kutoka
Pwani alilaumiwa na AFC kuwa aliwapa Pepsi bao ambalo sio halali pamoja na kuwanyima penalti, katika mchezo huo kocha mkuu wa timu ya AFC, Gerald Totoo alioneshwa kadi nyekundu kwa kuondoka eneo lake wakati mchezo ukiendelea.
Totoo alisema baada ya kurudi katika eneo lake alishangaa kuoneshwa kadi nyekundu wakati hakufanya jambo lolote baya kwa mwamuzi wala kwa kamisaa wa mchezo huo
“Baada ya kuona mwamuzi anachezesha sivyo nilimfuata kamisaa wa mchezo huo Babtise Mihafu aliyekuwa jukwaani na kumweleza jinsi ataharibu mchezo, kisha nikarejea kwenye benchi langu,” alisema Totoo.
Kocha huyo aliongeza kuwa, timu zinapaswa kuwa makini kwa kila mchezo hasa za Arusha ambazo zimehamia Moshi kwenye Uwanja wa Ushirika wasipokuwa makini itawagharimu.
No comments: