MTV watangaza majina ya wasanii kutoka Afrika watakaowania tuzo za MTV EMA 2017

Kituo cha runinga cha MTV kimetangaza majina ya wasanii watakaoiwakilisha Afrika katika tuzo za MTV Europe Music Awards 2017, kwenye kipengele cha Best African Act 2017, ambapo mwaka huu hakuna msanii hata moja kutoka Tanzania.
Kwenye orodha hiyo ya wasanii


watakaochuana ni Davido, Wizkid wote kutoka Nigeria, NastyC na Babes Wodumo kutoka Afrika Kusini, Nyansiski kutoka Kenya na C4 Pedro kutoka Kenya.
Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika jijini London, Uingereza tarehe 12 Novemba mwaka huu.
SOMA ZAIDI – Alikiba akabidhiwa tuzo yake ya MTV EMA
Tuzo ya MTV EMA 2016, kwenye kipengele hicho cha Best African Act mwaka jana ilichukuliwa na Alikiba kutoka Tanzania.
Unaweza kumpigia kura msanii wako HAPA na kuangalia orodha kamili ya majina ya wasanii wanaowania tuzo za MTV EMA 2017 HAPA .

No comments: