Wakati wanawake wengi weusi wakijitahidi kubadilisha ngozi zao kuwa weupe kwa gharama yoyote ile hii inakuwa tofauti kabisa na mawazo ya Mwanamitindo (Model) Martina Big kutoka Ujerumani .
Martina Big
Mrembo huyo ambaye alishawahi kuwa muhudumu wa kwenye ndege ‘Air Hostess’ alichukua uamuzi wa kubadilisha kabisa ngozi yake ya nyeupe akidai kuwa anapenda kuwa mweusi na huwa mara nyingi anaota kila anapolala kuwa yupo kwenye muonekano huo.
Martina (28) amesema alitumia dola $50,000 sawa na Tsh milioni 112 kwa kufanya upasuaji mdogo wa matiti na kubadili ngozi yake kabisa.
Martina Big kabla ya kubadilisha muonekano
Kwenye mahojiano yake na kituo cha ITV cha nchini Uingereza amesema yeye anaamini kuwa ndiyo alikuwa mwanamke mwenye matiti makubwa kuliko mwanamke yeyote barani Ulaya hivyo ameyaongeza ukubwa ili avunje rekodi barani Afrika.
“ Nilijiona mimi ndiye nilikuwa mwanamke mwenye matiti makubwa barani Ulaya ndipo nikaamua kuongeza ukubwa wa matiti na nimefanikiwa naamini naonekana kama wao ,”asema Martina.
Akiingia kwenye studio za ITV
Alipoulizwa swali na mtangazaji wa kipindi cha This Morning cha ITV, Phillip Schofield kuwa kwa nini amechukua uamuzi wa kubadili rangi yake, alisema kuwa anapenda kuwa mweusi na ni ndoto yake na anawapenda sana watu weusi.
“ Sipendi kabisa kukwazana na watu weusi na navutiwa na rangi zao nilikuwa nikiota kuwa kama wao na ndoto yangu imetimia, Najiona ni mwanamke mweusi na ndio maana nimepanga kuwa januari mwakani nitaenda Afrika kujifunza tamaduni za huko, “amesema Martina.
Martina alipoulizwa kuhusu mabadiliko hayo kufananishwa na vitendo vya ubaguzi wa rangi, amesema watu wengi wamekuwa wakimfikiria hivyo ila yeye hana lengo hilo na hajawahi kufikiria kuhusu ubaguzi wa rangi.
Martina amesema msukumo wa kubadilisha rangi yake umekuja baada ya kuvutiwa na muonekano wa Pamela Anderson na Katie Price.
“ Nataka nionekane kama mtoto ila niwe na matiti makubwa, kama Pamela au Katie mara ya mwisho nilipo onana nao nilikuwa mweusi na mwenye nywele nyepesi lakini kwa sasa nimekuwa mweusi na nywele ngumu najivunia ,”amesema Martina.
Hata hivyo mrembo huyo amedai kuwa kabla ya mwezi januari mwakani atafanya operation ndogo ya pua ili iendane na muonekano wa kiafrika na tayari rafiki yake wa kiume wa kiume amesha mruhusu kufanya ivyo.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa mchumba wa mrembo Martina aliyoyatoa kwenye mahojiano na gazeti la The Sun amesema mke wake alikuwa akichomwa sindano tatu kwa siku za kubadilisha rangi yake.
Mwanamke huyo amesema kwa sasa tayari mwili wake umeanza kukataa baadhi ya vyakula vya kizungu na ameanza kupenda muziki kutoka Afrika na Marekani.
No comments: