TIMU ya taifa ya Malawi imeshindwa kuifunga Tanzania iliyocheza pungufu ya wachezaji wawili, baada ya viungo wake, Erasto Nyoni na Muzamil Yassin kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili na kutoa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jioni ya leo.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Israel Mujuni Nkongo aliyeisaidiwa na Frank Komba na Soud Lila wote wa nyumbani, hadi mapumziko Malawi walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na Nahodha wa The Flames, Robert Ng’ambi dakika ya 35 kwa kichwa akiwa ndani ya boksi la wapinzani akitumia makosa mabeki wa Tanzania kurudishiana mipira kwenye eneo la hatari.
Pamoja na kuondoka uwanjani ikiwa nyuma kwa 1-0 baada ya mapumziko, lakini Taifa Stars ilipoteza nafasi kadhaa za kufunga ilizotengeneza.
Dakika ya tatu winga Simon Msuva anayechezea Difaa Hassan El- Jadida ya Moroco aliingiza krosi safi kwa Nahodha wake, Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji, lakini akachelewa na mpira kuwahiwa na kipa wa Malawi, Swini Charles
Stars ilipata pigo dakika ya 14, baada ya kiungo wake, Hamisi Abdallah anayechezea Sony Sugar ya Kenya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Muzamil Yassin.
Dakika ya 15 Msuva tena, aliingiza krosi nzuri lakni Samatta akachelewa hadi kipa wa Malawi akauwahi.
Malawi wakajibu dakika ya 19 baaad ya Phiri Gerald kupiga kona safi iliyokwenda moja kwa moja langoni kwa Stars, lakini sifa zimuendee kipa Aishi Manula aliyeokoa.
Msuva aliendelea kuwa mwiba kwenye ngomr ya Malawi baada ya dakika ya 26 kupiga krosi safi tena, lakini Nahodha Samatta akazidiwa ujanja na kipa wa Malawi, aliyefanikiwa kuruka na kuokoa hatari.
Nahodha Mbwana Samatta alikaribia kuifungia Taifa Stars bao la pili dakika ya 70 kama mpira wa kichwa aliopiga kuunganisha krosi ya Erasto Nyoni kugonga mwamba na kurudi uwanjani.
Refa Nkongo alimuonyesha kadi ya njano Mhango Gabadinho dakika ya 72 kwa utovu wa nidhamu baada ya kubishana naye na dakika ya 75 akempandisha jukwaani Kocha Mkuu Mholanzi wa Malawi, Ron van Geneugden kwa kosa la kuingia uwanjani.
Beki mkongwe wa Tanzania anayeweza kucheza kama kiungo pia, Erasto Edward Nyoni alitolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kwenda kumpiga mchezaji wa Malawi, Mbulu Richard aliyemchezea rafu mchezaji mwenzake wa Tanzania.
Mshambuliaji chipukizi, Mbaraka Yussuf akaunganishia nje kwa kichwa krosi ya Samatta dakika ya 88.
Muzamil Yassin akaonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 89 na kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Phiri Gerald wa Malawi.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Abdi Banda, Kevin Yondan, Himid Mao, Simon Msuva/Adul Hilal dk85, Hamisi Abdallah/Muzamil Yassin dk14, Mbwana Samatta, Raphael Daudi/Mbaraka Yussuf dk54 na Shiza Kichuya/Ibrahim Hajib dk58.
Malawi; Swini Charles, Gomezgan Chirwa, Lanjesi John, Chambezi Denis, Fodya Nyamkuni, Ngambi Robert, Phiri Gerald, Banda John/Bandawe Fretcher, Chirwa Chikoti, Mhango Gabadinho na Mbulu Richard.
No comments: