Kichwa cha mwandishi wa Sweden Kim Wall kimepatikana , miezi miwili baada ya kupotea katika ziara na raia mmoja wa Denmark.
Waogeleaji walipata mifuko iliokuwa na kichwa chake, miguu na nguo katika eneo la Koge Bay kusini mwa mji wa Copennhagen kulingana na inspekta mkuu wa polisi wa eneo hilo Jens Moller Jensen.
Vilipatikana karibu na pale mwili wa Wall ulipokuwa siku chache tu baada ya kupanda katika manuwari tarehe 10 Agosti.
Bwana Marsden mwenye umri wa miaka 46 amekana kumuua bi Moller Jensen akisema mabegi hayo yaliopatikana yalikuwa yamechanganywa na kupimwa uzani na vipande vya vyuma.
''Jana alfajiri tulipata begi ambalo lilikuwa na nguo za Kim, suruali ya ndani na viatu.katika begi hilo hilo kulikuwa na kisu na kulikuwa na mabomba ya magari'' .
Matokeo ya uchunguzi yamebaini kwamba kichwa hicho ni cha bi Wall na kwamba hakina ishara za kwamba fuvu lake la kichwa liliumizwa ama hata kupigwa.
Matokeo hayo yanaenda kinyume na taarifa za Marseden kwamba alifariki baada ya kugonga kichwa chake katika mlango.
Bi Wall ,30, alionekana mara ya mwisho akiwa hai jioni ya Agosti 10 wakati alipokuwa akiondoka na bwana Marsden katika manowari aliotengeza mwenyewe kuhusu habari aliokuwa akiandika kuhusu safari hatari aliotaka kufanya.
Mpenziwe alipiga kamsa siku ya pili baada ya kutorudi kutoka kwa safari yake.
Awali bwana Marsden alisema kuwa alimsafirisha na kumwacha akiwa salama mjini Copenhagen , lakini baadaye akabadilisha taarifa yake na kusema kwamba alimzika baharini baada ya ajali mbaya na alikuwa amepanga kujiuwa kwa kuizamisha manowari yake.
No comments: