WAKULIMA wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa wametakiwa kuacha kukataji miti mashambani bila kupata vibali vinavyowaruhusu kukata miti kutoka kwenye mamlaka husika kutokana na na katazo la sheria inayozuia ukataji miti bila kufuata utaratibu hata kama mti huo uliupanda mwenyewe.
Miongoni mwa vitendo vinavyochangia uharibifu mkubwa wa mazingira mkoani Rukwa ni ukataji miti kwa ajili ya kilimo, ufugaji, uwindaji na nishati ya mkaa na kuni na sasa wilaya ya kalambo imetoa elimu kwa wananchi juu ya taratibu za ukataji miti kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura amewataka wananchi kuzingatia sheria za maizngira kwani hivi sasa hali ya mvua na upatikanaji wa maji imeathiriwa sana na kazi za kibinadamu.
No comments: