Hii ndo Takwimu ya Tanzania dhidi ya malawi

Timu ya taifa ya Tanzania chini ya Kocha Salumu Mayanga leo inatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na timu ya taifa ya Malawi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotambuliwa na shirikisho la kandanda ulimwenguni FIFA.



Katika kuelekea mtanange wa huo timu ya taifa Tanzania inapigiwa upatu mkubwa wa kuibuka na ushindi kutokana na rekodi iliyonayo kwa mechi takribani sita taofauti huku kukiwa na kumbukukumbu za timu hizo kukutana na Tanzania kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Malawi.
Ifuatayo ni michezo 6 ya hivi karibuni ambayo kila timu imecheza.
Mechi 6 za Mwisho kwa Tanzania
Mechi tunayoanza nayo ni ya 28/03/2017 Tanzania ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi uwanja wa taifa Jijini Dar es salaam na Tanzania kuibuka na ushindi wa goli 2 - 1.
Mechi ya pili ni ya 25/03/2017 ambayo pia ilikua ya kirafiki na Tanzania iliibuka na ushindi wa goli 2 - 0 dhidi ya Botswana
Mechi ya tatu ni ya 07/09/2013 hii ilikua ya kufuzu kuahiriki kombe la duni kundi C ambapo katika mchezo huo Tanzania ilipoteza kwa kufungwa goli 2-0 ugenini dhidi Gambia.
Michezho mingine ni ile ya
16/06/2013 ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Ivory coast huku ikipoteza kwa goli 4 kwa goli 2.
08/06/2013 kufuzu kombe la dunia dhidi ya Morocco na Tanzania kupoteza kwa goli 2 kwa goli 1
24/03/2013 nyingine ni dhidi ya Morocco tena katika uwanja wa nyumbani na Tanzania kushinda 3 - 1 dhidi ya Morocco.
 Zifuatazo ni mechi 6 Za Malawi.
18/04/2017 mechi ya kirafiki dhidi ya kenya na zikatoa sare ya bila kufungana 0 - 0
07/09/2013 kufuzu kombe la dunia dhidi ya Nigeria na kupoteza kwa goli 2-0
12/06/2013 Kufuzu kombe la dunia ikatoa sare na kenya ya goli 2-2.
05/06/2013 kufuzu kombe la dunia sae dhidi ya Namibia 0-0
23/03/2013 kufuzu kombe la dunia na kushinda dhidi ya Namibia 1 - 0.
22/12/2012 mechi ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini 1 - 3 .
Hata hivyo Tanzania huenda ikatumia furusa ya kuchezea nyumbani kuinyuka Malawi.

No comments: