WANAMUZIKI wanaounda kundi linalotikisa Bongo kwa sasa la Rostam, Roma Mkatoliki na Stamina, wamefunguka kuwa, endapo mmoja kati yao akibaini mwenzake amechepuka, basi ndiyo itakuwa mwisho wa uhai wa kundi hilo. Wawili hao kwa sasa wanatamba na wimbo wao wa Huku Ama Kule ambao unafanya vizuri kwenye vituo vya redio na runinga.
Roma amesema: “Yaani sisi kila mtu hapa alipo anamlinda mwenzake kuhakikisha hapigi, hachepuki licha ya kwamba kuna vishawishi vingi ambavyo tunakutana navyo wakati tukisaka ugali wetu wa kila siku.
“Kama ikitokea siku m i m i nimemfuma Stamina au yeye akanifumania nipo na mwanamke mwingine tofauti na mke wangu tukifanya mambo ya kimapenzi, basi hapo ndiyo utakuwa mwisho wa kundi hili.”
No comments: