Mufti Zubeir amesema hayo kwenye mkutano uliofanyika leo (Jumapili) katika makao makuu ya bakwata yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mufti amesema kupitia sensa hiyo BAKWATA itaweza kupanga vyema mipango yake ya maendeleo pindi idadi halisi ya waislamu itakapojulikana.
Aidha Mufti Zubeir amewataka pia viongozi wa bakwata nchini katika ngazi mbalimbali kuepuka kufanya kazi kwa kugongana huku akiwataka kila mmoja kutimiza wajibu wake kama katiba ya BAKWATA inavyotaka
No comments: