Wakati kikosi cha Yanga kikiendelea na mazoezi kujiandaa na muendelezo wa ligi kuu huku nyota wake wengine wakiwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kinachoshuka dimbani Jumamosi kucheza dhidi ya Malawi, nyota wawili wa kikosi hicho hali zao zimewekwa wazi.
Mshambuliaji kutoka Burundi, Amissi Tambwe amerejea kujiunga na kikosi cha Yanga huku Mzimbabwe, Donald Ngoma akiendelea kusalia nje ya kikosi kutokana na majeraha yanayomsumbua.
Akielezea hali za nyota hao, Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kwamba kikosi kipo katika hali nzuri huku Amissi Tambwe akiwa amerejea kikosini na Donald Ngoma akiwa bado hajajiunga na kikosi hicho.
“Tambwe amerejea kikosini, Ngoma bado hali yake lakini hali za wachezaji zipo vizuri wakiendelea kufanya mazoezi na kocha huku wengine wakiwa kwenye kikosi cha timu ya taifa” alisema Ten.
Pia, Ten amesema kwamba kikosi cha Yanga kimewapandisha wachezaji watano kutoka kikosi cha pili ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho baada ya wachezaji wake wengine kujiunga na timu ya taifa.
“Kocha amewaongeza wachezaji watano kutoka kikosi cha pili ili kukiongezea nguvu kikosi chetu” alimaliza.

No comments: