Cristiano Ronaldo Auza tuzo yake ya D'OR Ballon soma sababu za kuuza..



Staa wa soka wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameamua kuuza tuzo yake ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or aliyoshinda mwaka 2013 ili kutoa msaada.
Ronaldo amefikia maamuzi ya kuipiga mnada tuzo yake hiyo kwa lengo la fedha zitakazopatikana achangie katika foundation ya
Make-A-Wish inayohusika na kusaidia watoto wenye magonjwa hatarishi.
Tuzo hiyo ya Cristiano Ronaldo imepigwa mnada na kununuliwa na bilionea wa Israel Idan Ofer kwa pound 600,000 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1.7 za kitanzania.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri hii sio mara ya kwanza kwa Ronaldo
kutoa msaada aliwahi kutoa bonus yake aliyopewa na Real Madrid baada ya kushinda Kombe la UEFA Champions League na kusaidia watu wasiojiweza.

No comments: