Wadau mbalimbali wa vyombo vya habari na taasisi za kiraia nchini Tanzania wanakutana Alhamisi jijini Dar Es Salaam kujadili kanuni za maudhui ya mitandaoni.
Mkutano huo ambao umefunguliwa rasmi na katibu mkuu wa wizara ya habari nchini Tanzania pia umehudhuriwa na wakurugenzi mbali mbali kutoka serikalini.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, katibu mkuu wa wizara prof. Elisante Ole Gabriel amesema, kutokana na kasi ya ukuaji wa matumizi ya mtandao, wakati umefika kuboresha kanuni za maudhui ya mtandaoni kwa lengo la kusaidia tasnia na wala sio kudhibiti.
Ameongeza kusema lengo la kuwashirikisha wadau mbalimbali ni kuepuka kutunga kanuni ambazo baadae zitakinzana na utendaji kazi.
Miongoni mwa wajumbe wanaohudhuria mkutano huo wa siku moja ni ma bloga, wamiliki wa mitandao na waandishi wa habari.
No comments: