Muungano wa upinzani nchini Kenya umeitisha maandamano ya umma kupinga mapendekezo ya kuifanyia mabadiliko sheria ya uchaguzi.
Wabunge wanaoegemea upande wa serikali wanafanya hima kupitisha mswada ambao utamwezesha Uhuru Kenyatta kutangazwa rais bila ya kufanyika uchaguzi ikiwa upinzani utasusia marudio ya uchaguzi tarehe 26 mwezi Oktoba.
Wanachama wa upinzani walitoka nje wakati upande wa serikali ukitumia wingi wake bungeni kuharakisha mabadiko ambayo yatasababisha mswada huo kuwa sheria kabla ya marudio ya uchaguzi.
Kati ya yale yaliyo kwenye mswada huo ni kuruhusu mgombea kutangazwa rais bila ya kufanyika uchaguzi ikiwa mgombea mwingine atasusia uchaguzi.
- Viongozi wa upinzani Kenya wazuiwa kwenye uwanja wa ndege Nairobi
- Upinzani kuandamana Kenya
- ''Zaidi ya 100 walifariki'' katika maandamano Ethiopia
Marudio hayo ya uchaguzi yana wagombea wawili, Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.
Mswada huo pia unasema kuwa mahakama ya juu haiwezi kufuta matokeo ikiwa mfumo wa eletroniki utafeli
Kufeli kwa mfumo wa kupiga kura kwa njia ya eletroniki ndio ilikuwa sababu kuu ya kufutwa kwa matokeo ya urais.
Mgombea wa Upinzani Raia Odinga amekashifu hatua hizo kama jaribio la kuiba kura na kumpendela rais Uhuru Kenyatta.
Ametisha maandamano ya kote nchini kila Jumatatu na Ijumaa kuanzia wiki ijayo
No comments: