Kijana wa miaka 17 Canada aitwaye Mo Omer amejitengenezea simu ya smartphone mwenyewe baada ya mama yake mzazi kumwambia kuwa hana uwezo wa kumnunulia simu ya aina hiyo.
Mo Omer baada ya kutengeneza simu hiyo ambayo anasema haijatofautiana chochote na smartphone za makampuni mengine ya simu ameanza kutengeneza asimu hizo na kuziuza kwa Dola za Marekani 180 ambayo ni kama Tsh 432, 000.
“Kutengeneza simu sio suala gumu au la kuchanganya kama watu wengine anavyofikiria na hadi sasa nimeshauza simu hizi maeneo mbalimbali ya Afrika kama Nigeria, Algeria na mengineyo.” – Mo Omer
No comments: