Serikali yaagiza nyumba ya mwekezaji kubomolewa


Naibu Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, William Tate Olenasha ameagiza nyumba ya mwekezaji iliyojengwa kwenye mfereji wa kupeleka maji katika mashamba ya wakulima wa ushirika Ruvu ibomolewe haraka ili kuruhusu maji kumwagiliwa mashambani.

Naibu Waziri huyo alitoa, agizo hilo leo alipokuwa ametembelea shamba la mpunga la kilimo cha ushirika Ruvu (CHAURU) ambapo alielezwa kuwa kuna mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji wa kichina aitwaye Guo Ming Tang ambaye aliingia mkataba batili na uongozi wa awali wa ushirika huo mwaka 2012 kwa niaba ya  CHAURU.

Mwenyekiti wa CHAURU, Sadala Chacha amemweleza Naibu Waziri kuwa  mgogoro huo umekuwa wa muda mrefu na kuwa kuziba mfereji huo kumesababisha ekari 24 kutokulimika  kwa miaka mitano na kusababisha upotevu wa  wastani wa kilo 236,000 za mpunga zenye thamani ya sh. 200,600,000.

Baada ya kuelezwa migogoro kadhaa kati ya wakulima na mwekezaji huyo, ikiwemo huo wa kuziba mfereji  na pia kuwauzia maji wakulima,ya kumwagilia kwa saa moja kwa bei ya sh. Laki moja naibu waziri alitoa maagizo kadhaaa  sambamba na kuvunjwa kwa nyumba hiyo ya mwekezaji

No comments: