Sakata la Neymar na Cavanni lazua mpya


Bado habari za Edison Cavanni na Neymar zinaendelea kutawala vichwa vya habari, baada ya mvurugano uliotokea wiki chache  zilizopita inasemekana wafalme hawa wawilu walipatana na Neymar aliomba msamaha.


Lakini sasa kumeibuka jipya, inasemekana mabosi wa klabu ya PSG walikaa chini na Edison Cavanni na kumuomba amruhusu Neymar kupiga penati huku pia wakitaka kumpa kiasi cha pesa ili kukubali.

PSG walitaka kumpa Cavanni kiasi cha €1million ambayo ni pesa ambayo wangempa Cavanni mwisho wa msimu kama akimalizia mfungaji bora lakini sasa wakataka kumpa kiasi hicho ili amuachie Neymar kupiga tuta.

Edison Cavanni amekataa kiasi hicho cha pesa na hii inamaanisha kwamba hayuko tayari kumuachia mtu mwingine apige penati na anaona ni bora akose kiasi hicho cha pesa kuliko kuacha kupiga penati.

Inadaiwa kwamba baada ya Neymar na Cavanni kugombana ilimbidi tajiri wa PSG Nasser El Khaifi kukaa na Cavanni ili kujaribu kumshawishi kuhusu kumpa Neymar penati lakini Cavanni amekataa.

Mbaya zaidi inadaiwa kwa sasa kumeanza kuwa na makundi katika klabu hiyo kwani kuna kundi kubwa ndani ya PSG linalomsuport Cavanni huku kikundi kingine kidogo kinachoundwa na Wabrazil pekea yao wakiwa wanamuunga Neymar.

Hali hii inamuweka njia panda kocha wa klabu hiyo Unai Emery kwani ni wazi na yeye anataka Cavanni aendelee kupiga penati katika timu hiyo lakini tajiri wa timu anaonekana anataka Neymar awe kila kitu.

No comments: