Patcho Mwamba ampiga chini mfanyakazi wake

Image result for Patcho Mwamba picha
PREZIDAA wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Patcho Mwamba ‘Tajiri’ amemtimua mwanamuziki Redock Mauzo baada ya ‘kuzinguana’ kuhusiana na maslahi.

Redock Ijumaa iliyopita alionekana akikamua kwenye jukwaa la BMM Sound katika onesho lililofanyika BMM Pub Mwenge jijini Dar na alipoulizwa ilikuwaje kuikacha bendi ya FM Academia akasema walishindwana kutokana na maslahi.

“Sipo tena Ngwasuma hii ni baada ya kuzinguana na Patcho kuhusu maslahi yangu akasema kama nataka niondoke ndipo nikaona isiwe shida ndiyo nikaja kupiga kazi na BMM,” alisema Redock.

Alipou-lizwa Prezidaa Patcho kuhusiana na hilo, alisema hayo yameshapita asingependa kuyazun-gumzia

No comments: