Neymar Jr ajishusha kwa Edinson Cavani na kuiomba clab yake ya PSG msamaha
Magazeti Ufaransa yanasema mshambuliaji Neymar Jr ameomba msamaha kwa Edinson Cavani na wachezaji wenzake wa Psg kwa kile kilichotokea wiki iliyopita.
Mbrazil huyo aliingia katika mgogoro na Cavani kwa kugombania kupiga penati na “free kick” katika mchezo dhidi ya Lyon jumamosi iliyoisha.
Baada ya mechi wawili hao waligombana katika vyumba vya kubadilishia nguo na baadae Neymar kumu-Unfollow Cavani katika Instagram na kufanya kuzua maneno zaidi.
Gazeti la L’Equipe la Ufaransa limeripoti Neymar ameomba msamaha kwa wachezaji wenzake jana jumatano mazoezini huku Nahodha wao Mbrazil Thiago Silva akisimama kama Mkalimani
No comments: