Staa wa Filamu Berry amepigwa picha akiwa na mpenzi wake Alex Da Kid ambaye ni mtayarishaji maarufu wa muziki Marekani.
Halle Berry ambaye ni kawaida yake kutoka na vijana wadogo au aliowapita umri kwa sasa anatangaza filamu mpya ya Kingsman 2: The Golden Circle, huku mapaparazzi wakimsumbua kuhusu kuwa na mahusiano na kijana huyu Alex da Kid.
Halle Berry ana umri wa miaka 51 na mpenzi wake ana umri wa miaka 35, Huyu Alexander Grant, a.k.a. Alex da Kid ni producer kutoka London Uingereza na ameshafanya kazi na wasanii kama Dr. Dre, Nicki Minaj, Eminem na Diddy
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na tovuti ya SeekingArrangement, asilimia 42 ya wanawake wanakuwa na mahusiano na vijana wadogo kutokana na nguvu zao
No comments: