Mwendesha mashtaka mkuu nchi Kenya aamrisha tume ya uchaguzi IEBC ichunguzwe

Mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya, Keriako Tobiko, ameamuru uchunguzi ufanywe dhidi ya tume ya kusimamia uchaguzi nchini Kenya IEBC.
Hii ni kuhusiana na makosa yaliyofanyika wakati ilipokuwa ikishughulikia uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita.
Bwana Keriako Tobiko ameiomba idara ya polisi pamoja na tume ya kupambana na ufisadi nchini humo, kuwasilisha kwake ripoti ya uchunguzi huo katika kipindi cha siku 21 zijazo.
Pia amewaomba kuchunguza madai kuwa, maafisa wawili wakuu wa muungano wa upinzani nchini Kenya, walifaulu kudukua kompyuta za tume ya uchaguzi.
Mwendesha mashtaka mkuu nchi Kenya aamrisha tume ya uchaguzi IEBC ichunguzwe
Hiyo inafuatia uamuzi wa mahakama ya juu zaidi nchini Kenya kufutilia mbali uchaguzi wa Urais wa Agosti nane kwa madai kwamba kulikuwa na makosa chungu nzima, huku mahakama hiyo ikikataa kuwalaumu moja kwa moja maafisa wakuu wa tume hiyo kwa kufanya makosa.
Tarehe ya Uchaguzi mwingine imetangazwa kuwa Oktoba 26.

No comments: