Taasisi ya Jakaya Kikwete inayojihusisha na kutibu maradhi ya moyo JKCI imepata ugeni kutoka nchini India na imeanza kuanza kutoa mafunzo ya kutibu maradhi mbalimbali ya moyo kwa madaktari nchini ili kuboresha upatikanaji wa matibabu hayo na kupunguza watu kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge ameeleza kuwa wataalamu wa afya wamepokea mafunzo hayo kutoka kwa madaktari bingwa kutoka India ili kuweza kuanza kutoa huduma za matibabu ya moyo nchini na haya ni mafanikio makubwa kwenye sekta ya afya na serikali kwani itapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za matibabu ya moyo.
No comments: