MourinhoTutakosa huduma ya wachezaji muhimu dhidi ya CSKA

Klabu ya Manchester United leo usiku itaingia uwanjani kuvaana na watukutu wa Urusi timu ya CSKA Moscow katika michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya.
Image result for jose morinho
United itaingia katika mchezo huo wa michuano ya  UEFA Champions League ambayo ni mikubwa kabisa ya soka inayoshika nafasi ya pili baada ile ya kombe la dunia huku ikikosa huduma ya Paul Pogba, Marouane Fellaini na Michael Carrick .
Meneja wa United, Jose Mourinho ambaye timu yake haijapoteza katika michezo nane iliyoingia uwanjani amesema kuwa watakosa huduma ya viungo wake muhimu dhidi ya CSKA.
”Fellaini ni mchezaji muhimu ndani ya Old Traford kwakuwa ni mwenye bahati”, amesema Mourinho.
Mourinho ameongeza ”Sitokuwa na Fellaini, Pogba na Carrick, kwa hivyo viungo wakati wote watakosekana katika mechi hii”.
Wachezaji, Carrick na Fellaini hawatakuwepo katika mchezo huo kutokana na majeraha waliyo yapata katika mshikemshike wa Ligi Kuu ya Uingereza wakati Pogba akikosekana kutokana na kukaanje kwa muda mrefu.

No comments: