Mwanamke mmoja nchini Italia aliyetambulika kwa jina la Laura Mesi, amejioa mwenyewe na kisha kufanya shereke kubwa, baada ya mahusiano yake yaliyodumu kwa miaka 12 kuvunjika.
Sherehe hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu 70 huku akiwa na wasindikizaji wake, haikuwa ya kisheria lakini amesema alifanya hivyo ili kutimiza ndoto zake, na kuonyesha jinsi gani anajipenda mwenyewe.
Laura amesema mawazo ya kujioa mwenyewe yalimjia miaka miwili iliyopita, ambapo aliwaambia marafiki zake kuwa iwapo atafikisha miaka 40 bila kupata mwenzi, basi atajioa mwenyewe.
“Niliwaambia marafiki zangu na familia yangu kwamba iwapo sitompata mwenzi mpaka natimiza miaka 40, nitajioa mwenyewe”, alisikika Laura akimwambia mwandishi mmoja nchini humo.
Miss Laura ameendelea kuwama kwamba ..”Iwapo siku moja nitampata mwanaume ambaye nitaweza kupanga naye maisha ya baadaye nitafurahi, lakini faraja yangu haimtegemei yeye”.
Watu wanaounga mkono suala hilo wamesema kitendo hicho ni sawa na kujionyesha upendo mwenyewe na kujikubali.
Bi Laura amesema yeye ndio mwanamke wa kwanza kufanya hivyo nchini Italia, ambapo mwezi Mei mwaka huu, mwanaume mmoja amefanya hivyo.
No comments: