Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa Uganda ambaye kwa sasa ni kocha Orlando Pirates ya Afrika kusini, Milutin 'Micho' Sredojevic amejipanga kurudi upya katika mchezo wao dhidi ya Timu ya Polokwane, baada ya kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya mabingwa watetezi Bidvets Septemba 23 katika ligi kuu ya nchini Afrika Kusini.
Micho amesema wanatambua kuwa walipoteza katika mechi za awali lakini kwa wanatazama mbele zaidi ili kuweza kupata matokeo mazuri.
Orlando Pirates na Polokwane watashuka katika dimba la Peter Mokaba, Jumamosi nchini Afrika Kusini.Kocha micho amesema Msimu huu haujawa mzuri kwao na ameliona hilo lakini amedai atahakikisha wanajipanga na kupata matokeo mazuri.
Ameongeza kusema hata kama wakipata matokeo mazuri ambayo wanahitaji wanatakiwa kuyaweka na ikitokea wamepata matokeo mabaya wanatakiwa wasahiishe zaidi
No comments: