Mchezaji tenis muingereza, Kyle Edmund ambaye anashika nafasi ya 46 katika viwango vya ubora wa mchezo huo duniani ameibuka na ushindi dhidi ya Bernard Tomic katika michuano ya wazi ya Chengdu ‘Chengdu Open’ nchini China.
Edmund ambaye amerejea uwanjani kwa mara ya kwanza toka apate majeraha amemshinda muaustralia huyo kwa jumla ya seti 6-4 6-2.
Katika michezo mingine inayopigwa Jumatano ya leo muhispainia Albert Ramos atakipiga dhidi ya Lajovic , Julio Peralta dhidi ya Michael Venus huku Peter Gojozyk akikipiga na Leonardo Mayer.
No comments: