Breaking News: Nyumba za polisi zawaka moto mkoani Arusha


Nyumba za Jeshi la polisi mkoani Arusha zilizopo Kata ya Sekei Arusha zinawaka moto muda huu huku juhudi za kuendelea kuzimwa moto huo zikifanyika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. Kazi ya kuzima moto huo inaendelea Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo pia yupo eneo la tukio.

No comments: