Fahamu Athari Za Kisaikolojia Zinazomkumba Mtoto Anayelelewa Na Mzazi Mmoja

 Mzazi mmoja ni nani? ni mtu ambaye amefiwa na mume au mke  na kuachiwa malezi ya watoto peke yake.

Pia mzazi mmoja anaweza kuwa mwanamke au msichana aliyepata ujauzito bila kufunga ndoa, hapa anaweza kuwa mwanafunzi wa sekondari, shule ya msingi au wa Chuo Kikuu.

Pia kwa maisha ya siku hizi wanawake wenye uwezo kimaisha hupendelea kulea watoto wao bila msaada wa mwanaume aliyezaa naye kwani wengi wao hukwepa kuingia kwenye maisha ya ndoa kwa sababu mbalimbali.



 ATHARI ZA KISAIKOLOJIA

Uchunguzi uliofanywa na wanasaikolojia umebaini kuwa mtoto mwenye umri kati ya miaka mitatu hadi mitano hasa wa kiume huwa karibu sana na mama na watoto wa kike wenye umri huo pia huwa karibu zaidi na baba, kutokana na ukaribu huo watoto hao watakuwa na mapenzi hata wakija kuingia kwenye mahusiano pale wanapokuwa wamevunja ungo au kubalehe hukosa uelekezi mzuri kwenye tabia chanya.

Kukosa ukaribu; watoto hasa kwenye kipindi cha kubalehe au kuvunja ungo ndio athari zinaanza kujionesha kwani kuna vitu ambavyo anatamani kumueleza na mzazi husika kama ni baba au mama ili kuweza kupata taarifa husika, lakini pale anapokosa maelekezo ya mzazi ananza kutafuta taaarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii ambayo itamsababisha kutopata uhalali wa jambo analotarajia kulifahamu.

Athari ya kiuchumi; hapa anazungumziwa mzazi asiye na uwezo wa kutimiza mahitaji ya mwanae kutokana na kudorora kwa uchumi ambapo hupelekea mtoto kuathirika kisaikolojia kwa kukosa mahitaji muhimu shuleni kama viatu, sare za shule na ada. Hali hii inayompelekea unyonge mtoto huyu kitaalamu huitwa (Inferiorty Conflict) ambayo huathiri namna ya kujifunza.

Kupata kasoro za kisaikolojia kwenye jamii; hapa mtoto ambaye anapata malezi ya mzazi mmoja anakosa kujiamini hata mbele za watu kwani  hakupata malezi ya pande zote mbili hali inayochangia kufifisha uwezo wake wa kujiamini.

No comments: