Muongizaji wa video Bongo, Ivan ametuhumiwa na kumtapeli kiasi cha shilingi milioni mbili msanii wa muziki aitwaye Ericom kwa kutofanya video yake.
Akiongea katika ENewz ya EATV, Ericom amedai kuwa alimpatia Ivan kiasi cha pesa kwa ajili ya utengenezaji wa video ila ilivyotoka video hiyo haikuwa na thamani sana na kiasi cha pesa alichompatia.
“Ivan alipewa pesa kimakubaliano ambapo ilitakiwa ifanyike kitu kivuzi kutokana na project ilikuwa ni project kubwa akapewa kiasi kadhaa cha pesa tukakubaliana fresh ila mwisho wa siku ikawa tena sio kufanya yeye tena video yani kifupi akazindua yani kuna director ambaye yeye yupo naye ikabidi yulke director kwa moyo wake wa huruma kuana suala limesha kuwa kubwa ikabidi aingilie kati akasema bhana ngoja tuy nikusaidie kufanya video na katika kunisaidia kufanya video inamaana tukatoa tena gharama nyingine ambazo zikawa tofauti na zilezilizotoka,” amesema msanii huyo.
Pia akaongeza ” Vitu vingine sitaki kusema au sio bhana ila ninacho mshaurini ilituendelee kuonana vizuri tukikutana barabarani tunasalimiana tuna peana hi arudishe mpunga na mimi kweli boss wangu anone huyu mtu alifanya hivi na hivi .”
No comments: