Bunge lamjibu Mbowe

 Ofisi ya Bunge imekanusha taarifa zilizokuwa zinaenea katika mitandao ya kijamii na kusema haijampokonya gari Kiongozi wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe bali walimtaka dereva wa gari hiyo arudi Tanzania ili aweze kufuata kibali

Taarifa hiyo imekuja baada ya Mkuu wa idara ya Uenezi CHADEMA, Hemedi Ali kudai gari ambalo alilopewa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe  na Bunge kwa ajili ya mizunguko yake mbalimbali, ambayo pia ilikuwa akiitumia mjini Nairobi nchini Kenya kwenye matibabu ya Lissu imenyang'anywa na Bunge.

"Ni vema ieleweke kuwa ni kweli gari yenye Na. STL. 4587 Aina ya Toyota Prado imetengwa maalum kwa ajili ya kumuhudumia Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika kutekeleza Majukumu yake ya kikazi na binafsi hapa Nchini.

Mbowe aliomba gari ikamhudumie Mjini Nairobi nchini Kenya ambapo ofisi ya Bunge iliridhia ombi hilo na kuomba taratibu zizingatiwe. Hata hivyo, ofisi iligundua kwamba gari ilikwenda Nairobi na dereva hakupata kibali cha kusafiri nje ya nchi ambacho kila mtumishi wa umma anayesafiri nje ya nchi lazima apate kibali hicho kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi (Chief Secretary)", imesema taarifa hiyo.

Kwa muendelezo wa habari hii soma hapa chini.

No comments: