Yanga SC yabanwa mbavu, Azam FC yakwea kileleni VPL

Michezo kadhaa ya Ligi Kuu Tanzania Bara imepigwa hii leo katika viwanja mbali mbali wakati katika uwanja wa Uhuru Mabingwa watetezi Young

Africans imetoka sare tasa ya bila kufungana dhidi ya vinara wa Ligi timu ya Mtibwa Sugar, ‘Wakata Miwa wa Manungu, Turiani, Morogoro’.
Huko mkoania Dodoma Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC imekubali kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida United, kwa matokeo hayo sasa timu hiyo yenye maskani yake Chamazi inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa tofauti ya magoli dhidi ya Mtibwa Sugar ambao wametoa sare ya bila kufungana na Yanga SC.
Klabu ya Mbao FC imetoshana nguvu ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, wakati Mbeya City wakicheza na Mwadui wametoka sare ya mabao 2-2.
Na klabu ya Ndanda FC imechomoza na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya timu ya Lipuli FC wakati Ruvu Shooting ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Njombe Mji.
Katika mechi zote 7 za leo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara sita hazijatoa mshindi, huku Ndanda FC pekee ikiondoka na pointi 3.

No comments: