Watu 2 wauawa kwenye shambulizi la kisu Ufaransa
Watu wawili wameuawa kwenye shambulizi la kisu katika kituo cha treni cha Saint Charles huko Marseille nchini Ufaransa, kwa mujibu wa vyombo vya habari.
Mshambuliaji aliuawa na maafisa wa usalama kwenye mji huo ulio Kusini mwa Ufaransa.
Waziri wa mashauri ya ndani nchini Ufaransa, Gérard Collomb, anasema anaelekea eneo hilo.
Polisi waliandika katika mtandao wa twitter kuwa hali imethibitishwa na mshambuliaji kuuliwa.
Afisa mmoja wa polisi ambaye hakutajwa jina aliliambia gazeti la Le Monde kuwa mshambuliaji alitamka maneno "Allahu akbar".
No comments: