Afisa habari wa klabu ya Simba sports, Haji Sunday Manara ameonyeshwa kufurahishwa na matokeo ambayo klabu yake imeyapata katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya Stand United uliopigwa katika uwanja wa CCM Kambarage pale mjini Shinyanga.
Katika mchezo huo Simba imeibuka kwa ushindi wa goli 2-1 kwa magoli ya Shiza Ramadhani Kichuya na lile la Laudit Mavugo, huku goli la kufutia machozi la Stand United likipachikwa kambani na Mutasa Munashe mnamo dakika ya 52.
Haji ameandika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii wa instagram unaonyesha kufurahishwa na matokeo hayo ambayo yameiwezesha klabu hiyo kujinyakulia pointi tatu zilizoipeleka klabu hiyo kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara.
"Alhmdulilah, muhumu tumepata points tatu leo, Unawajua hao madogo?? Simba raha sana"... Amesema Haji Manara.
No comments: