STAA namba moja katika Hip Hop kwa sasa nchini, anayetamba na kibao na video yake ya Zimbabwe, Ibrahimu Musa a.k.a Roma Mkatoliki, amesema licha ya usafi kuwa ni muhimu, lakini mtoto wa kiume anastahili kuoga angalau mara mbili tu kwa siku.
Akipiga stori na Risasi Vibes, Roma alisema anapenda kuwaona vijana watanashati, lakini linapokuja suala la kuoga, kama ni lazima, basi angalau aoge mwisho mara mbili kwa siku, vinginevyo, inaleta ukakasi na kuondoa tabia za kiume.
“Kusema ukweli mwanaume kuoga angalau iwe mara mbili tu kwa siku, si vema mtoto wa kiume unaoga kutwa mara nne au tano, inaleta ukakasi na kwa upande wangu huwa namtazama mwanaume wa aina hiyo kwa jicho lenye maswali mengi ndani yake,” alisema.
No comments: