Kocha Wa Zaman Wa Manchester United Atua Bayern Munich..


Aliyekuwa kocha mkuu wa Manchester United Louis Van Gaal anaripotiwa kumrithi Carlo Ancelott kuifundisha klabu ya Bayern Munich nchini Ujerumani.
Ancelot ametimuliwa katika kikosi cha wababe hao wa Bundesliga wiki iliyopita baada ya kupigwa 3-0 na Paris-saint Germaine kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Van Gaal ni kipindi cha miaka miwili sasa toka aondoke viunga vya Old Traford jijini Manchester na kujiweka kando na soka , sasa anatajwa kuja kuiongoza Bayern mpaka mwishoni mwa msimu huu wa 2017-18 endapo watakubaliana vyema kwa vikao vinavyoendelea .
Louis Van Gaal mwenye umri wa miaka 66 hii itakuwa sio mara yake ya kwanza kuifundisha Bayern bali alifanya hivyo pia kuanzia mwaka 2009 mpaka 2011 alipotimuliwa. Aliweza kushinda mara mbili kombe la ligi kuu na kuifikisha timu hiyo fainali ya klabu bingwa Ulaya.
Mahusiano mabovu ya Van Gaal na raisi wa Bayern Uli Hoeness kilikuwa chanzo kikubwa kwa mdachi huyo kutimuliwa katika kikosi hicho jambo ambalo linashangaza hivi sasa Uli kumtaka Van Gaal kuokoa jahazi la timu hiyo.
Jumanne ya wiki hii Uli Hoeness alifanya kikao cha siri na rafiki yake kipenzi kocha wa Manchester City Pep Guardiola kumjua mrithi wa Carlo Ancelott. Baada ya kikao hicho kilichofanyika Bavarian, Uli aliutangazia umma kwamba ni Pep ndio anajua nani anakwenda kuifundisha timu hiyo.
Kocha Thomas Tuchel aliyewika na Borrusia Dortmund baada ya kikao hicho alisikika sana akitajwa kuingia Allianz Arena kutokana na urafiki mkubwa kati yake na Pep mshauri wa Uli Hoeness lakini pia hapo ndipo lilipoibuka jina la Louis Van Gaal na Julian Nagelsmann. Lakini Van Gaal anatajwa kubeba asilimia 100 kuchukua mikoba ya Ancelott kwa kipindi hiki kifupi.

No comments: